
Wakimbiaji wa Marekani wakiwa wenye furaha kwenye mtandao wa Snapchat
Kamati ya Olimpiki ya Marekani imeomba radhi kwa raia wa Brazil kwa kile walichosema jambo lisilokubalika la waogeleaji wa Marekani waliodai kuwa waliiibiwa huko Rio.
katika taarifa yake timu hiyo ya Marekani imesema kwa jinsi wanavyolifahamu tukio hilo mmoja wa waogeleaji aliharibu choo kwenye moja ya vituo vya mafuta.
Polisi wa Rio wanasema mmoja wa waogoleaji hao alikubali kuwa taarifa kuwa walivamiwa na kuibiwa hazikuwa za kweli.
Wawili kati ya waogeleaji hao waliohojiwa na polisi na hawakuruhusiwa kuondoka kutoka mjini Rio.
