» » » Zaza aandika ujumbe Instagram uwafikie Waitaliano wote

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


 Usiku wa Jumapili kwenye mchezo wa robo fainali kati ya Italy na Ujerumani, mshabulizi wa Italy Simone Zaza alipiga moja ya penati mbovu kabisa kuwahi kutokea katika michuano ya Euro.

Suala lake limekuwa likiongelewa sana kutokana na ukweli kwamba, Antoinio Conte alimuingiza kwa lengo maalum kwa ajili ya mikwaju ya penati.

Ujumbe wa Instagram wa Simone Zaza kwenda wa Waitaliano wote

Nazidi kuomba mshamaha kwenu kwa kusema nisameheni kwa kwaangusha watu wote ambao walikuwa na imani kubwa na sisi lakini mwisho wa siku wakapata maumivu kwa matokeo ya timu yetu.

Napenda kusema kuwa siku zote timu yetu inatambua kwa kiasi kikubwa na imefarijika sana mchango wenu. Huu ni ukweli usiopingika.

Wote ambao wamekuwa wakitoa sapoti bila ya kujali matokeo ya timu, nawashukuru sana.

Na vile vile wote ambao kabla ya mchezo wanatizama macho yetu na kutufanya tuamini hatupo 23 pekee bali ni idadi kubwa ya watu.

Ningependa kuwashukuru watu wote ambao walinisapoti baada ya tukio hili na ningependa hili mlifahamu.

Na zaidi ya yote, napenda kusema kwamba mimi ni shabiki namba moja wa taifa hili, hivyo kwa nimefadhaika, nimehuzunika na kupata hasira kubwa juu ya kilichotokea, nimefarajika kuona na sisi noimoja ya mataifa ambao mashabiki wake wana mwamko na imani kubwa kwa wachezaji wao.

Kilichotokea kitaendelea kubaki nafsini mwangu milele.

Penati ile ilikuwa ni kwa faida ya timu na mimi mwenyewe. Lakini nikashindwa.

Pengine miaka michache watakuwa wakikumbuka tukio hili na sio kukumbuka wachezaji 23 waliokuwepo kwenye kikosi ambao walijitahidi kupigana kila hatua kuhakikisha timu inafanya vizuri.

Lakini hili ndiyo soka na ndivyo lillivyo.

Nisameheni kwa mara nyingine tena

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post