» » » Yanga yaahirisha kupiga kambi nje ya Dar .......ni baada ya kukosa sehemu stahiki.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Klabu ya Yanga imeahirisha kuweka kambi nje ya Dar kwa ajili ya maandlizi ya mchezo wao wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Meadeama baada ya kukosa sehemu stahiki.

Awali ilitajwa kwamba wangeenda Pemba, lakini walipokwenda kuomba uwanja wa Gombani ambao ndiyo huwa wanautumia wakiwa huko, wakakuta uwanja huo unafanyiwa matengenezo.

Sehemu nyingine ilitajwa kuwa ni Mbeya, lakini huko nako kukaonekana kuna hali ya baridi ambayo kiufundi ingewapa shida kwenye mchezo wa marudiano watakapowafuata Medeama baada ya mchezo wa Julai 16 kwenye uwanja wa taifa.

“Tulipanga kwenda Pemba kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wetu wa Julai 16 dhidi ya Medeama lakini uwanja ambao huwa tunautumia kwa mazoezi tukiwa huko tumearifiwa kwamba uko katika matengenezo,” alisema kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm.

“Mbeya ingekuwa sememu nzuri kwa ajili ya kuweka kambi lakini kutokana na hali ya hewa ya baridi ya huko, inaweza ikatuletea shida kwenye mchezo wetu wa marudiano tutakaposafiri kwenda Ghana kucheza mchezo wa marudiano.”

Yanga wanajipanga kuingia kambini leo au kesho hapahapa Dar na watakuwa wakijifua kwa kutumia uwanja wa Boko Veteran au uwanja wa taifa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post