RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB, Profesa William Lyakurwa kuanzia jana na amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kushika nafasi hiyo.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu, kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa, Rais amechukua hatua hiyo kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha Sheria ya Tafsiri za Sheria Sura 1.
“Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya Mashirika ya Umma Sura 257, Rais amemteua Profesa Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, ilieleza kuwa kutokana na mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kwa mamlaka aliyonayo, ametengua uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB. Kutokana na hatua hiyo, Dk Mpango amewateua wajumbe wapya wa bodi kwa miaka mitatu.
Wajumbe hao ni Brigedia Jenerali mstaafu Mabula Mashauri, Dk Razack Lokina, Rose Aiko, Profesa Joseph Bwechweshaija, Said Seif Mzee, Dk Arnold Kihaule, Maduka Kessy na Charles Singili.
Benki ya Maendeleo ya TIB zamani ikijulikana kama Benki ya Rasilimali Tanzania ni benki inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania. Ilianzishwa mwaka 1970 na imekuwa ikitoa mikopo ya muda wa kati na muda mrefu katika sekta za kilimo, uzalishaji, usindikaji, ujenzi, utalii na madini.