ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Wachaji wa Ureno
Ureno imekuwa nchi ya kwanza kuingia fainali ya michuano ya Euro baada
ya kuzima ndoto za Wales kwa kuichapa magoli 2 - 0 katika mechi ya nusu
fainali mjini Lyon nchini Ufaransa.
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa mwiba kwa
wapinzani kwenye mashindano hayo baada ya kupachika goli kabla
mshambuliaji wa zamani Manchester United Luis Nani kupigilia msumari wa
moto kwenye kidonda kwa kupachika goli la pili.
Kwa matokeo hayo Ureno sasa itakutana na mwenyeji Ufaransa au Ujerumani katika mechi ya fainali.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO