Tanga.Watoto 13,266 wenye umri chini ya miaka 10 wa wilaya tatu za mkoani Tanga wamenufaika na huduma za afya zinazotolewa na taasisi moja ya Korea ya United Help for International Children, ( UHIC).
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kanda ya Tanzania, Lee Kwiwoon ametoa taarifa hiyo katika mkutano uliowajumuisha madaktari, manesi na wahudumu wa afya kutoka wilaya za Muheza,Tanga na Pangani zilizounganishwa katika mradi huo.
Kwiwoon amesema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutoa huduma kwa watoto wenye matatizo ya kiafya yanayowapata hasa wale wenye umri chini ya miaka 10.
Kwa mujibu wa Kwiwoon, watoto wengi wenye umri chini ya
miaka 10 hukumbwa na magonjwa ya malaria, upungufu wa damu, utapiamlo, kifua na kuharisha huku wengine wakiwa wamezaliwa njiti.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Rehema Maggid alisema watoto 653 wamepoteza maisha kutokana na magonjwa mbalimbali, yakiwamo malaria, kikohozi, upungufu wa damu na kuharisha.
Hata hivyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa waTanga, Mayassa Hashim amesema ana matumaini kwamba ujio wa taasisi hiyo utasaidia kuepusha vifo visivyotarajiwa kwa watoto wadogo.