Akizungumza jana katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama amesema kama sheria hiyo itatungwa itawafanya watoto hao kutojihusisha na ngono kwa kuhofia kufungwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti ukimwi katika halmashauri hiyo, Benedictor Manuari ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha yanakuwa na takwimu sahihi za wagonjwa wa Ukimwi pamoja na kupeleka elimu ya kujikinga na maambukizi vijijini.
Amesema kama elimu hiyo itaendelea kutolewa kwa kasi, uwezekano wa kumaliza tatizo hilo ni mkubwa.
