» » Rufaa mauaji ya bilionea Msuya Agosti 3

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Moshi. Rufaa mbili zilizokatwa dhidi ya uamuzi wa Jaji anayesikiliza kesi ya mauaji ya bilionea, Erasto Msuya zitasikilizwa Agosti 3 katika Mahakama ya Rufani.

Rufaa hizo mbili, namba 74/2016 iliyokatwa na upande wa Jamhuri na namba 106/2016 iliyokatwa na washtakiwa saba katika kesi hiyo, zitasikilizwa jijini Arusha  na Jopo la majaji watatu.

Pande zote katika kesi hiyo hazikuridhishwa na uamuzi mdogo uliotolewa Januari 26, mwaka huu na Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo inavuta hisia za watu wengi.

Ratiba iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Eddie Fussi inaonyesha jopo hilo la majaji linaundwa na Jaji Edward Rutakangwa, Angela Kileo na Salum Masati.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post