» » » Mpira mwingi wa Mahadhi wamtikisa Busungu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

MALIMI Busungu amepona majeraha yake aliyopata katika mechi ya kimataifa baina ya Yanga na GD Segrada Esperanca ya Angola, lakini kumbe akiwa anajiuguza alimpiga chabo kimtindo winga mpya wa timu hiyo, Juma Mahadhi.

Anakiri ni kweli Mahadhi ni mtamu sana, lakini yeye haangalii kiwango cha winga huyo na badala yake anajifua ili kuhakikisha analiondoka benchi lililoanza kumzoea Jangwani tangu aliposajiliwa kutoka Mgambo JKT.

Busungu alisema kwa kujiamini; “Nimesajiliwa Yanga, kuonyesha ushindani kuisaidia timu, siwezi kuanza kubabaika na kiwango cha Mahadhi, nadhani ni fursa aliipata na ameifanyia kazi, hilo kwangu halinisumbui hata kidogo naangalia yangu,” alisema.

Mkali huyo alisema kuwa kwa sasa amepona majeraha ya mgongo na jana Alhamisi  ameungana na wenzake katika mazoezi ambapo alidai kuwa anajipanga kujifua vikali ili arejeshe kiwango chake halisi.

“Narejea kivingine msimu ujao kwani sijaona kama kuna mtu anayeweza kunishinda kwenye ushindani wa namba ila najua upepo kama haujakukalia vema ndiyo hivyo unaonekana kama umefulia, bado nipo fiti, siwezi kuisha mapema hivi,” alisema.

Naye Juma Mahadhi alisema anatambua kwamba amejichongea kwenye ushindani wa namba hivyo anajipanga kuhakikisha anapata mafanikio ya kufanya vizuri ndani ya kikosi cha kwanza cha kocha wake Hans Pluijm.

“Siwezi kuridhika kwa kiwango ambacho nilikionyesha katika mechi moja dhidi ya TP Mazembe, nitaendelee kujifunza kwa bidii kutoka kwa wakongwe ambao wana uzoefu ndani ya kikosi hiki najua ipo siku nitafikia malengo yangu ila si kazi rahisi,” alisema.

Mahadhi aliyesajiliwa akitokea Coastal Union alipiga mpira mwingi katika pambano la Yanga dhidi ya Mazembe katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni mchezo wake wa kwanza na vijana wa Pluijm kabla ya kuumia na kutolewa nje.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post