» » Kabla ya Kuwasili Tanzania Waziri Mkuu wa India amefanya safari ya kihistoria ya treni

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amefanya safari ya kihistoria ya treni katika siku yake ya mwisho ya ziara yake nchini Afrika Kusini ikiwa ni kumbukumbu ya safari iliyofanywa na kiongozi wa uhuru wa India Mohandas Gandhi .

Modi ambaye tayari alikutana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ikiwa ni sehemu ya ziara yake barani Afrika yenye lengo la kuimarisha mahusiano katika nyanja za kibiashara na masuala ya kiusalama, pia amekutana na jamii ya Waafrika Kusini wenye asili ya Kihindi waishio nchini humo.

India inatafuta njia za kujiimarisha kibiashara zaidi barani Afrika ambako mshindani wake kibiashara China imewekeza kwa kiwango cha juu zaidi, ambapo nchini Afrika kusini amesaini makubaliano ya kushirikiana katika nyanja za teknolojia ya habari na mawasiliano na kuahidi kushirkiana katika sekta za madini, ulinzi na dawa.

Katika ziara hiyo barani Afrika Waziri Mkuu Narendra Modi anawasili nchini Tanzania leo na badaye kwenda Msumbiji na Kenya.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post