Jumla ya wanamichezo kumi na mbili wa timu ya Tanzania ya Olimpiki wakiwemo wanariadha, waogeleaji, wachezaji wa judo, makocha na matabibu wanatarajiwa kuondoka nchini mwezi wa nane mwaka huu kueleka jijini Rio nchini Brazil.
Kutajwa kwa kikosi hicho kunaashiria ni wazi kuwa mabondia Thomasi Mashali na Amosi Mwamakula waliokua wakijiandaa kwenda Venezuela kushuiriki michuano ya kufuzu kuelekea Brazil wamekosa nafasi hiyo.
Hapo jana rais wa Shirikisho la Masumbwi Tanzania Muta Rwakatael aliomba wadau mbalimbali kuwasaidia kwa hali na mali mabondia hao waweze kupata nauli ya kwenda kushiriki mashindano hayo.