Misungwi. Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumkata mapanga, Mpelwa Mbiti (65) kwa kinachosadikiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia Julai 7, Kitongoji cha Shitonga, Kijiji cha Buhanda wilayani Misungwi wakati mwanamke huyo alipokuwa amelala na mjukuu wake, Leticia Bundala.
Mmoja wa watoto wa Mbiti, Maria Kasubi (40), amesema kabla ya mauaji hayo walisikia vitu vikirushwa juu ya paa.
“Mtoto wangu wa kiume, Faustine John alitoka nje na kumulika kwa tochi juu ya paa lakini hakuona kitu na kurejea ndani,” amesema Kasubi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema msako na upelelezi wa kina kuhusu mauaji hayo umeanza na kuahidi wahusika wote watatiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani.