» » Zitto amchachamalia Magufuli

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


ZITTO Kabwe, kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ametoa tamko lake juu ya kauli ya Rais John Magufuli ya kupiga marufuku vyama vya siasa kufanya shughuli za kisiasa zaidi ya bungeni na kwenye kampeni za mwaka 2020 ni sawa na kuua demokrasia.

Tumepokea kwa MSHTUKO na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa kampeni na kupitia bungeni.

Tunaichukulia kauli ya Rais kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya nchi na namna ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya demokrasia nchini mwetu.

Tunatoa wito kwa vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita hii pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria.

Tunatoa wito kwa wananchi wote na taasisi za kiraia kusimama imara katika kulinda demokrasia. Tunasisitiza kuwa ushahidi wa kisayansi unaonyesha kuwa huwezi kuua demokrasia bila kuua juhudi za maendeleo. Tusiruhusu mtu yeyote mwenye mamlaka kuua demokrasia nchini mwetu.

Hatua zozote za kuua demokrasia ni kuua Umoja, Amani na mshikamano wa wananchi na Taifa, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yetu kijamii, kisiasa na kiuchumi. Tunatoa wito kwa wananchi wote kushikamana na kusimama imara katika kulinda demokrasia.

Zitto Kabwe, MB
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post