India radi
Watu 53 walifariki katika jimbo la Bihar.Watu 10 waliuawa katika jimbo la mashariki la Jharkhand huku wengine 16 wakifariki katika eneo la Madhya Pradesh.
Wengi waliuawa walipokuwa wakifanya kazi katika mashamba yao wakati huu wa msimu wa mvua
Ni idadi kubwa sana ya watu kuuawa kwa mpigo mmoja ,jambo ambalo limewashangaza wengi.
Katika muongo uliopita, zaidi ya watu elfu mbili wamefariki kwa kupigwa na radi kote nchini India.
Ni vigumu sana kubashiri ni lini janga la radi litatokea na si rahisi kwa utawala kutoa tahadhari ya kutokea kwa radi.
