» » Wagonjwa wanaolazwa wametafutiwa huduma Chakula Muhimbili

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam imeanzisha utaratibu mpya wa utoaji huduma ya chakula kwa wagonjwa wote wanaoolazwa ambapo kila mgonjwa atachangia shilingi elfu hamsini kwa kipindi ambacho atakuwa amelazwa.

Kati ya fedha hizo shilingi elfu 10000 zitakuwa ni gharama ya kulazwa, elfu 10,000 nyingine gharama ya kumuona daktari huku shilingi elfu 30000 ikiwa ni za gharama ya chakula kwa milo mitatu.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha mawasiliano hospitali ya taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha amesema licha ya kuchangia shilingi elfu 30 kwa chakula ambayo itahisha kipindi chote ambacho mgonjwa atakuwa amelazwa, gharama halisi ya chakula ni shilingi 6000 kwa siku.

Amesema kufuatia uamuzi huo, kuanzia Julai 1 mwaka huu utaratibu wa ndugu na jamaa kupeleka chakula mchana kwa mgonjwa hospitali utafutwa rasmi hivyo mchana hakutakuwa na fursa ya ndugu na jamaa kutembelea wagonjwa.

Wakati huo huo kaimu mkurugenzi mkuu wa hospitali ya taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru  ametolea ufafanuzi juu ya wagonjwa wa selimundu.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na wagonjwa wa HIV Profesa Museru amesema wagonjwa hao wanaendelea kutibiwa bure ila tu kama watapata magonjwa nyemelezi ndipo inabidi kutibiwa kawaida kama wagonjwa wengine.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post