» » Wa miaka 65 ampa mimba mwanafunzi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Hai. Mzee  wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nkuu Kisereny mwenye umri wa miaka 65  amempa ujauzito binti mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Nkuu iliyopo maeneo ya Machame wilaya ya Hai.

Hali hiyo imezua taharuki baada ya wananchi wenye hasira kali, hususani wazee kujitoa kumtafuta mtuhumiwa, huku wakidai kuwa wamechoshwa na vitendo vyake vya kuwarubuni mabinti wadogo kwa kuwapatia vizawadi vidogovidogo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Ndelilio Mwenda alisema binti huyo alibainika kuwa na ujauzito wa miezi sita baada ya upimaji kufanyika katika moja ya zahanati zilizopo Machame na  alipohojiwa alimtaja mzee huyo ambaye alisema ni mjomba wake.

“Kama ilivyo kawaida agizo la upimaji mimba kwa wanafunzi hufanyika kila mara na ni agizo la lazima kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa,”alisema Mwenda.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post