
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Jaji Mohamed Gwae anayesikiliza shauri hilo baada ya upande wa utetezi unaowakilishwa na mawakili Robert Kidando na Obadia Kajungu kuweka pingamizi ukiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa madai ina mapungufu kisheria.
Katika hoja zao mawakili hao wanaowawakilisha wadai wawili, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanadai mleta maombi (Chadema) kupitia kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho hawakunukuu kifungu cha 5(1)(2) ambacho kingeipa Mahakama mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusiana na ombi hilo.
