Dar es salaam. Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imesema wapangaji zaidi ya 1,700 kati ya 3,000 katika nyumba za serikali wanadaiwa wastani wa Sh3.4 bilioni.
Kauli hiyo ameitoa leo mbele ya waandishi wa habari, wakati wa usafi wa nyumba za TBA, Mikocheni ikiwa ni sehemu ya kufunga maadhimisho ya Wiki ya Utumishi Umma nchini.
Kwa mujibu wa TBA, tangu Machi mwaka huu deni hilo lilikuwa wastani wa Sh6 bilioni lakini hadi Juni mwaka huu baadhi ya wateja wamelipa Sh 2.6 bilioni.
Mtendaji Mkuu TBA, Elius Mwakalinga amesema ulipaji huo umeanza kuonekana baada ya kutumia nguvu ya kutaka kuwaondoa kwenye makazi hayo.