» » Tanzania na Uganda zatakiwa kusitisha uwindaji

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Arusha.Serikali ya Tanzania na Uganda, zimeshauriwa kusitisha kwa muda uwindaji wa kitalii wa tembo ili kudhibiti matukio ya ujangili ambayo yanaendelea kupunguza idadi ya wanyama hao duniani.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elephant Neighbors Center ya Kenya, Jim Nyamu ametoa wito huo wakati akiongoza matembezi ya kilomita 3,200 katika nchi za Afrika ya Mashariki kupinga mauaji ya tembo ambayo yamefika Arusha.

Matembezi hayo yameanzia Nairobi Kenya kwa kuzinduliwa na Mke wa Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta, Margaret na yanatarajiwa kufika jijini Dar es Salaam Julai 6 na kupokewa na Mke wa Rais John Magufuli, Janeth  na baadaye kuendelea nchini Uganda.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post