» » Polisi Wakamata Risasi 853 Zilizofichwa Kwenye Dumu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

ESHI la Polisi mkoani Morogoro, limekamata risasi 853 zinazotumika kwenye silaha aina ya G3 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye dumu la lita 20 pembeni mwa mto Ngerengere eneo la Kihonda.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira ametoa taarifa kwa waandishi wa habari  akisema risasi hizo zilikamatwa jana jioni eneo la Kihonda Kilimahewa.

Rwegasira amesema polisi wakiwa katika utekelezaji wa mapambano dhidi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kwa kufanya msako maeneo mbalimbali ndipo walipopata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna risasi zimehifadhiwa na watu wasiojulikana pembezoni mwa mto huo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post