» » Odinga aanika yote waliyoteta na Uhuru

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Nairobi, Kenya. Rais Uhuru Kenyatta wiki hii alikutana kwa mara ya kwanza na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga kujadiliana juu ya hali ya kisiasa.

Hata hivyo, Odinga kwa wiki hii alijitokeza hadharani na kuzungumzia majadiliano yao na Rais Uhuru.

yaliyofanyika Ikulu mjini Nairobi.

Hiyo  ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanasiasa hao kukutana ana kwa ana tangu kuanza maandamano yanayofanywa na wapinzani wakishinikiza kubadilishwa kwa maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC).

Odinga alisema jana kuwa wamekubaliana kuendelea na majadiliano kwa ajili ya kumaliza utata unaoendelea.

Alisema kwenye majadiliano hayo yaliyodumu kwa muda wa saa nne, walikubaliana kuunda timu itakayoshughulikia kukwamua mzozo unaendelea kujitokezanchini humo.

“Napenda kusisitiza kuwa, mimi na Rais Uhuru tumekubaliana kuanzisha mazingira yatakayotusaidia kuondokana na hali hii,” alisema kiongozi huyo wa Muungano wa CORD na kuongeza.

Alisema yiko tayari kuapa mbele ya Biblia kwamba  wamefanya kile ambacho walikubaliana na wapinzani wao na wako tayari kuanzisha majadiliano nje ya Bunge.

Alidokeza kuwa moja ya makubaliano waliyofikia na Rais Kenyata ni kuvunja tume ya uchaguzi iliyopo na kuunda nyingine mpya.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post