
UZALISHAJI WA TIKITIMAJI
Tikitimaji ni zao la kitropiki linalo tumia miezi mitatu
kutoka kupandwa hadi kuvunwa.
ENEO
Chagua eneo ambalo halina historia ya kuwa na magonjwa ama
wadudu wanaoshambulia tikiti maji.Eneo ambalo maji yanapatikana kwa urahisi kwa
ajili ya umwagiliaji wa tikiti maji litafaa,pia eneo lisilo na udongo wenye
chumvi chumvi ama maji yenye chumvi chumvi.
KUANDA SHAMBA.
Lima shamba lako vizuri kwa kuvunja vunja udongo na pia
andaa matuta yenye upana wa mita 2 na urefu kwenda juu sentimita 30 ili
kusaidia mizizi ya tikiti kukua vizuri na kuzuia maji kutwaama hasa katika
kipindi cha mvua.
MAHITAJI YA TIKITIMAJI
Tikiti linakua vizuri ktk udongo unaoshika maji vizuri
lakini yasio tamwa na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji.Udongo wenye pH
5.8-6.6.
Tikiti halistawi vyema ktk baridi na linahitaji joto la
udongo kiasi cha 18-29 0c.
Joto chini ya 18 0c na juu 29 0c litaathiri kuota kwa mbegu
na ukuwaji wa mmea.Katika kipindi cha ukuwaji tikitimaji linahitaji unyenyevu
wa udongo wakati wote lakini maji yakizidi ktk udongo wakati wowote wa ukuwaji
na uwekaji wa matunda hupelekea upasukaji wa matunda na kupunguza mavuno na
ubora wa matunda.
UPANDAJI
Mbegu/mche wa tikiti maji utapandwa mita 1-2 kati ya mmea na
mmea na uwekwa sentimita 2.5 kwenda chini, na kati ya mstari na mstari iwe mita
2,kwa umbali huu panda mbegu 2 kila shimo.Au weka umbali wa sentimita 50 kwa
mita 2 lakini hapa panda mbegu moja moja.
Mbegu ya tikitimaji utokeza baada ya siku 5-7.
UTUNZAJI WA MMEA.
a) Mbolea.
Mbolea ya samadi kwa kiasi cha 4-6 tani kwa ekari,ichanganye
na udongo wiki kadha kabla ya kupanda,pia mbolea hii unaweza iweka katika kila
shimo siku kadhaa kabla ya kupanda kisha mwagilia ili kupunguza kiasi kikubwa
kitakacho hitajika kuweka ktk ekari moja.Kama huna samadi tumia Yaramila winner
au DAP weka gram 5 kwa kwa kila shimo ,hakikisha mbolea na mbegu havigusani.
Wiki mbili baada ya miche yako kutokeza weka mbolea ya
kiwandani -N-P-K (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila shimo,hakikisha
unaichimbia chini na isigusane na mmea.
Weka mbolea yenye Calcium kana Yaramila nitrabo gram 10 kwa
kila shina unapoona matunda yameanza ili kusaidia kupata matunda makubwa na
mazuri.
UMWAGILIAJI
Maji kwa sentimita 1-5 katika udongo yanatakiwa kwa mvua ama
umwagiliaji ili kupata tikitimaji zuri,kipindi cha muhimu sana kwa mahitaji ya
maji kwa tikitimaji ni :kabla ya mche kutokeza ,mwanzo wa kutoa maua na siku 10
za mwisho kabla ya kuvuna.Maji machache kipindi cha kupanda husababisha kutoota
kwa mbegu,kipindi cha kuweka maua husababisha
matunda machache kutokeza na matunda kukosa maumbo yake.Siku 10 za kuelekea
kuvuna husababisha matunda kuwa madogo kama maji ya kutosha
yasipopatikana.Matunda yakielekea kuiva punguza umwagiliaji maana kiasi kikubwa
cha maji kitasababisha kiasi kidogo cha sukari kutengenezwa na kupasuka kwa
matunda.
Angalizo:
Usimwagilie jion sana hii itasababisha kukua kwa magonjwa
kwa sababu ya kuacha majani ya mmea yakiwa na unyevunyevu .Pia angalia wakati
mzuri wa uchavushaji /wakati ambao nyuki
wanakuwepo shambani mwako hivyo jitahidi kumwagilia mda ambao hautawasumbua
nyuki.
Matandazo.
Ni muhimu kutumia matandazo ktk shamba lako ili kusaidia
kutunza unyevunyevu ktk udongo na matandazo haya baadaye yakioza uongeza rutuba
ktk udongo na pia kusaidia kuzuia kumea kwa magugu na husaidia tunda kutogusana
na udongo kitu ambacho kinaweza sababisha tunda kuathiliwa na joto la udongo
ama magonjwa kirahisi.Weka matandazo pale mche wako utakapo fikia urefu wa
sentimita 10.
Punguza urefu wa mmea
Ili kupata matunda mazuri na yenye afya ni vema kuupunguza
mmea kwa mbele ,pale unapoona mmea umefika urefu wa kutosha ili kusaidia
kutengeneza matawi ya pembeni ambayo mara nyingi ndio ubeba maua ya kike.
Kuondoa magugu
Ni muhimu sana kuondoa magugu ktk shamba lako hasa wiki za
mwanzo ili kuzuia ushindani wa mahitaji
kati ya magugu na mmea ambapo hupelekea kupungua kwa mavuno na muda mwingine
magugu haya yanaweza kuwa ndio chanzo cha baadhi ya magonjwa ktk mmea wako
Uchavushaji
Ili kupata kiasi kikubwa cha matunda ni vyema kuwa na mzinga
wa nyuki karibu na shamba lako ili kusaidia uchavushaji wa maua ya
tikitimaji.Waweza pia pands alizeti jilani na shamba lako ili kuvuta nyuki.Pia
zuia kupulizia dawa za wadudu kipindi cha maua maana unaweza wakimbiza ama waua
nyuki
Punguza idadi ya matunda
Kwa kawaida tikitimaji uweka zaidi ya matunda manne ,ili
kupata matunda makubwa na yenye afya ni vyema kupunguza matunda kwa kuondoa
baadhi ya matunda ambayo yanaonekana hayana afya nzuri na yaliopoteza umbo zuri
na kuhakikisha kila mche unabaki na matunda 2-3 tu.
Uvunaji
Tikitimaji uvunwa baada ya miezi mitatu kutoka siku ya
kupanda,lakin yapo ambayo hukomaa kwa siku 60-75 kutokana na aina ya mbegu.
Mangonjwa
1) Ubwiru chini (Downy mildew)
Huu ungonjwa husababishwa na fangasi
(Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na
hupendelea sana wakati wa baridi,
Dalili zake:
Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano
huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka
na madoadoa meus kwa mbali..
Tiba yake.
Tafuta dawa yenye viambato...Metalaxyl na mancozeb ....kama
vile Ridomil gold.
2) Ubwiru juu (Powdery mildew )
Dalili za huu ungonjwa...utaona majani yanakuwa kama
yamemwagiwa unga ua majivu
Tiba yake
Tafuta dawa yenye kiambato...Difenoconazole ..kama vile
Score.
3) Kata kiuno.(Damping off)
Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo,huanzia aridhini
,husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.
Tiba yake.
Tafuta Ridomil gold na anza kupulizia mara tu baada ya mimea
yako kuota.
Wadudu..
1) Wadudu mafuta (Aphid)
Hawa hushambulia majani na kufyonza juis ya mmea na baada ya
kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea mangonjwa ya virusi.
Dawa yao.
Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo.
Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.
,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec
itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.
Mbegu bora za
tikitimaji.
Kuna mbegu chotara na opv(Sio chotara)
But mbegu bora ni chotara na baadhi ya hizo mbegu ni...
1) Arashani F1-kutoka syngenta
2) Sukari F1-Kutoka East Africa seeds.
3) Sugar king F1-kutoka africasia
4) Juliana F1-kutoka Kiboseed
5) zebra F1-Kutoka Balton.
6) Pato F1-Kutoka Agrichem
Pia kuna ingizo jipya
Mbegu bora ya tikiti kutoka uswis sasa iko madukani tena kwa
bei ya promotion ...fanya haraka kuorder kabla ya promotion kuisha. ..bei ya
promo ni Mbegu 1000 ni Tsh 60 000.
Jina la mbegu ni Arashani F1-kutoka Syngenta.
Tikiti dogo kabisa ni kilo 8 na kubwa kabisa ni kilo 18 but
wastani ni kilo 14.
SOKO LA TIKITI
Napenda kuwashauri wakulima wetu kuwa
njia nzuri ya kulima tikitimaji ni ile ya umwagiliaji, ukiwa mkulima wa
tikitimaji lazima uwe mjanja kupanda zao lako ili uje uvune wakati soko
liliwa vizuri, mzunguko mzuri wa kupanda tikiti ni huu, panda zao lako
katikati ya msimu wa mvua wakati walimaji wa matikiti kwa kutegemea mvua
(ambao ni wengi) mazao yao yametoa maua ili wakati wao wanavuna tikiti
zao, mazao yako yawe ndio yanaanza kutoa maua kwa hiyo wakati unavuna
wakulima wa kutemea mvua watakuwa washamaliza soko lao.Pia kwa wale
wanaotegemea mvua ni vizuri uchunguze soko lako vizuri ili uwe na
uhakika wa kuuza matunda yako wakati yakiwa tayari yamekomaa.
