» » Mtu mmoja afariki dunia na wengine kunusurika katika ajali mkoani Ruvuma.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mtu mmoja asiyefahamika aliyekuwa akiendesha baiskeli amefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Haice huku abiria zaidi ya kumi waliokuwa kwenye gari hiyo iliyokuwa ikitoka Songea kwenda Peramiho wakinunusurika kufa baada ya ajali hiyo iliyotokea maeneo ya Mfaranyaki mjini  Songea mkoani Ruvuma.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hilo ni mwendo kasi uliomshinda dereva wa gari hilo ambapo alimgonga mwendesha baiskeli na kusababisha kifo chake  na kisha kumjeruhi mwendesha boda boda aliyelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma.

Kufuatia ajali nyingi kutokea eneo hilo la Mfaranyaki katika daraja la Mkomi wananchi wameiomba serikali kuweka matuta kwenye eneo hilo ili kudhbiti mwendo wa madereva huku wakiwalalamikia madereva wanaokimbiza magari kwa ajili ya kuwahi abiria  na kusababisha ajali.

ITV ilienda katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kuwaona majeruhi wa ajali hiyo ambapo akizungumza kwa simu na ITV Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk Philisy Nyimbi amesema waandishi hawaruhusiwi kuwaona majeruhi bila yeye kuwepo na  kwamba muda  huo haukuwa wa kazi huku Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw.Zuberi Mwombeji alipopigiwa simu yake ya mkononi alikuwa hapatikani....
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post