
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya anayefanya vizuri, Malaika Exavery
amesema anakerwa na kitendo cha watu wengi kumfananisha na muigizaji
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na gazeti hili, Malaika alisema huko nyuma alipokuwa
akifananishwa na msanii huyo hakujali, lakini kadiri siku zinavyozidi
kwenda imekuwa ni shida hadi wengine wanamsimamisha.
“Unajua kufananishwa na mtu siyo tatizo, lakini kwa hali ilivyo hivi
sasa lazima mtu usikie kuchoka kabisa kwa sababu hata wakati mwingine
unaendesha gari mtu anakusi mamisha halafu akikuangalia usoni vizuri
anaondoka, anasema alidhani ni Lulu,” alisema Malaika.
