Mlinga alitoa kauli hiyo wakati akiomba mwongozo wa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, akisema mbunge wa Chadema, Anathopia Theonest alimvua kofia ya balaghashia aliyokuwa ameivaa.
Mlinga alidai kuwa mbunge huyo alifanya kitendo hicho wakati wabunge wa Ukawa walipokuwa wanatoka nje kuendelea na msimamo wao wa kususia vikao vinavyoendeshwa na Dk Tulia. Alidai kuwa Theonest alimfuata na kumvua kofia yake, ambayo kwa mujibu wa kanuni za Bunge ni lazima ivaliwe na kanzu.
Alisema kitendo hicho ni cha udhalilishaji, kimetikisa akili yake, kimevunja amri ya tisa ya kutamani mume wa mtu mwingine, kimewakosesha wananchi wa jimbo lao uwakilishi wa muda aliokuwa nje ya ukumbi na kimedhalilisha vazi hilo.
