
Kadi za kieletroniki kwa ajili ya wasafiri wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam zitaanza kutolewa leo katika juhudi za kupunguza msongamano wa kununua tiketi za karatasi.
Wauzaji wa tiketi hizo MaxMalipo na Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA kitengo chake cha mradi wa mabasi yaendayo haraka wamesema tiketi hizo za kieletroniki zitauzwa katika vituo vikubwa kwa shilingi elfu tanio na mnunuzi atahitaji kusajil ili hata kama kadi yake itapotea akiba ya fedha iliyokuwa imebaki iingizwe kwenye kadi mpya atakayopewa.
