
shaffihdauda.co.tz imepiga story na kiungo huyo mkabaji mara baada ya mazoezi ya mwisho leso asubuhi ambaye amesema mchezo wa kesho utakua mgumu lakini ni mchezo muhimu kwa Stars kushinda.
“Game ni ngumu lakini ni game muhimu, mwisho wa siku inabidi tu-fight, tupambane na tupate matokeo”, amesema Himid ambaye kwa sasa anafanya vizuri kwenye nafasi ya kiungo wa ulinzi ambayo zamani ilitawaliwa na wachezaji wakongwe kama Shabani Nditi na Athumani Idd ‘Chuji’.
“Watu wote wako focused wana concentrate wako tayari kwa game, kwahiyo mchezaji atakayepata nafasi ataweza kufanya vizuri”.
Himid anaamini Stars itafanya vizuri kwenye mchezo wa kesho licha ya mchezo huo kuwa mgumu kutokana na nafasi ya Stars na Misri kwenye kundi.
