Mwanza. Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahamed Msangi amesema pamoja na
kuwaachia watu ambao hakutaja idadi yao, bado wanafuatilia wengine
ambao wanaonekana kuhusika na tukio hilo, bila kutaja idadi ya watu
waliochiwa.
“Wapo baadhi walioachiwa, wengine watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya kuona ushahidi una kila aina ya dalili za kuhusika na tukio hilo,’’ amesema Msangi.
Katika mauaji hayo, watu watatu waliuawa kwa kukatwa mapanga wakisali msikitini akiwamo Imamu wa Msikiti huo, Feruz Ismail na wengine wawili na kumjeruhi mtoto wa miaka 13.