ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Gari lilivyopata ajali.
Songea, Ruvuma
MTU mmoja ambaye hakufahamika jina lake aliyekuwa akiendesha baiskeli
amegongwa na gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace na kufa papo hapo
maeneo ya Mfaranyaki mjini Songea mkoani Ruvuma leo.
Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari la polisi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, gari hilo lilikuwa
na abiria zaidi ya kumi waliokuwa lilikuwa likitoka Songea kwenda
Peramiho, na chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni mwendo kasi uliomshinda
dereva wa gari hilo ambapo alimgonga mwendesha baiskeli na kusababisha
kifo chake na kisha kumjeruhi mwendesha boda boda ambaye alikimbizwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.
Gari lilivyopata ajali.
Kufuatia ajali nyingi kutokea eneo hilo la Mfaranyaki katika Daraja la
Mkomi, wananchi wameiomba serikali kuweka matuta kwenye eneo hilo ili
kudhbiti mwendo wa madereva huku wakiwalalamikia madereva wanaokimbiza
magari kwa ajili ya kuwahi abiria na kusababisha ajali.
Aidha Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk Philisy Nyimbi methibitisha
kupokea majeruhi wa ajli hiyo na kusema kwamba wanajitahidi kadri ya
uwezo wao kuwahudumia ili wapone.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO