» » Wapigwa vibaya na Wakala misitu baada ya Kuingia hifadhini

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

WATU watatu wamepigwa na kuumizwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao  na maafisa wa wakala wa misitu  Tanzania  wa wilaya ya Geita  (TFS)   huku mtoto Getruda Cosimas 16 akijeruhiwa vibaya mikono yake yote kwa kile kinachodaiwa kuingia hifadhini bila kibali.

Tukio hili la kusikitisha limetokea May 13 mwaka huu majira saa saba mchana katika pori la Chibingo lililoko kata ya Nyamigota  wilaya na Mkoa wa Geita.

Wakizungumza na  Channel Ten ndugu zake pamoja na mashuhuda wamesema kuwa mtoto wao alikwenda kuokota kuni lakini walishangaa kupigiwa simu na wasamalia wema kwamba mtoto wao amepigwa na maafisa misitu na kutupwa  kutelekezwa polini na hapa wanaeleza.

Diwani kata ya Rudete pamoja na mwenyekiti wa mtaa huo wamelaani kitendo walichofanyiwa wananchi huku wakiomba vyombo  vinavyousika kuchukua hatu kwa waliofanya .

Pamoja na kwamba majeruhi watatu ambao hawakutambulika majina yao mara moja kwenda katika kituo cha polisi Katoro na kupewa PF3 NO KTR /RB/890/2016. ili wakatibiwe  katika kituo cha afya Katoro walikolazwa siku tatu, cha kushangaza kaimu mganga mkuu Kilunga P. Kilunga amesema yeye hajui lolote huku meneja misitu Wilaya ya Geita Shadrack Msila akijitetea.

Jeshi la polisi Mkoani Geita limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba faili limefunguliwa ili kubaini waliofanya kitendo hicho.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post