
Wimbo huo umeandikwa na Lollypop ambaye pia aliandika nyimbo za Barakah Da Prince, Siachani Nawe na Nivumilie pamoja na Basi Nenda ya Mo Music.
“Sasa hivi kwanza nimepigisiwa simu na wasanii wengine wanaomba namba ya Lollypop,” Ben ameiambia Bongo5. “Hiyo ni kitu ambacho nilikuwa nataka kiwe hivyo,” ameongeza.
Ben Pol amesema tofauti na wasanii wengi, haoni kama ni kitu cha aibu kuandikiwa wimbo na mtu mwingine ambaye msanii atamtaja mara zote. Amedai amegundua kuwa sifa zote za uzuri wa wimbo huo anazipata yeye kama muimbaji hivyo hakuna kitu cha kuonea aibu kuandikiwa nyimbo.
“Hamna weakness ambayo naificha au labda nikautoa ule wimbo nikaficha baadhi ya details. Watu wengi wanafanya hivyo, wengi sana na nyimbo kubwa kweli, mtu anatoa nyimbo lakini hazungumzii kipengele cha nani kaandika, anazungumzia mambo mengine tu.”
