» » "Msiumizwe Komando Nipo Napigana"- Lady Jaydee

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Jay dee ameyasema hayo alipokuwa akiongea East Africa Televishion, na kusema kuwa muziki ni kila kitu kwake, na hajioni yeye bila muziki.

"Mafanikio yangu mpaka kufika hapa naweza nikasema ni nidhamu niliyonayo kwenye kazi yangu, nauheshimu sana muziki, kwani ni kila kitu kwangu, sijioni mimi bila muziki, hivyo nauthamini sana", alisikika Lady jay dee akisema.

Jay dee ambaye kwa muda alikuwa kimya kwenye muziki na kuibuka na wimbo wa NdiNdiNdi ambao umepokelewa vizuri, amesema hakutarajia kama NdiNdiNdi ungekuwa wimbo mkubwa, kwani hakuwa kabisa na hisia za kutoa kazi yoyote kwa muda huu.

"Unajua baada ya kukaa kimya, sikuwa na hisia ya kuandika wimbo wowote, nikakaa na watu Seven, akaandika, na kuna mtu mwingine kutoka Uganda nae akaandika, lakini waliandika mashairi ambayo walijua nitauvaa uhusika ipasavyo, zikaandikwa na nyingine lakini NdiNdiNdi ndo ikapitishwa itoke, hata sikufikiria ingekuwa kubwa, lakini nashukuru watu wameipokea vizuri sana", alisema jay dee.
Pamoja na hayo Jaydee ambaye amejielezea yeye ni mwanamke mpole lakini ana hasira pale anapokosewa, amewataka mashabiki wake wasiwe na wasi wasi na wasiumizwe na lolote, kwani komando wao yupo vitani anapigana.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post