» » Klabu kuadhibiwa kwa sababu ya viti Uhispania

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Klabu za Barcelona na Real Madrid zamani zilifaidi sana kutokana na mikataba ya runinga

Wasimamizi wa Ligi ya Uhispania wanapanga kuanza kuadhibu klabu ambazo zitaruhusu viti visivyo na mashabiki kuoneshwa kwenye runinga.

Hilo litaanza kutekelezwa kuanzia msimu ujao.

Kanuni mpya zinazitaka klabu za ligi kuu kuhakikisha maeneo yanayoangaziwa na kamera za runinga yamejaa mashabiki.

Lengo la hatua hii ni kuhakikisha viwanja vinavutia zaidi kwa watazamaji na pia kuongeza ushindani wa La Liga dhidi ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Mei 2015, Uhispania ilipitisha sheria mpya za kuwezesha haki za kupeperusha mechi kuunganishwa na kuuzwa pamoja kama fungu moja.

Awali, klabu kama vile Real Madrid na Barcelona zilikuwa zikijitetea kivyake na kupata mikataba ya thamani kubwa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post