» » Katumbi ashtakiwa kwa kuwaajiri mamluki DRC

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Tajiri mmoja wa mchezo wa kandanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Moise Katumbi ameshtakiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni,msemaji wa serikali amesema kulingana na chombo cha habari cha AFP.

Bw Katumbi alitangaza wiki mbili zilizopita kwamba atawania urais katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Msemaji wa serikali Lambert Mende aliambia AFP kwamba agizo la kukamatwa kwa Katumbi ambaye ndiye mmiliki wa kilabu ya TP Mazembe tayari limetolewa.

Bwana Katumbi awali alikana madai kwamba amekuwa akiwaajiri mamluki wa kigeni kuwa ya uongo na kwamba yalilenga kumzuia kuwania urais katika uchaguzi unaotarajiwa nchini humo.

Haijulikani iwapo uchaguzi utafanyika mnamo mwezi Novemba na iwapo rais Joseph Kabila anapanga kuondoka uongozini baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post