
Mtu mmoja ameripotiwa kupigwa risasi nje
ya uwanja wa Ikulu ya Marekani baada ya kukaribia kituo cha ukaguzi na
bunduki na kukataa amri ya kuishusha.
Taarifa zinasema mtu huyo alipelekwa hospitali ya George Washngton University akiwa
katika hali mbaya, inasemekana alipigwa risasi baada ya kukataa amri
iliyotolewa mara kadhaa ya kumtaka ashushe silaha aliyokuwa nayo.
Katika tukio hilo hakuna mwingine
aliyedhurika, vyanzo vya habari kutoka Serikali ya Marekani vinasema
maafisa wa usalama walikuwa wakimtazama mtuhumiwa na alikuwa hajaingia
ndani ya Ikulu hiyo.
Mmoja wa Afisa wa Ikulu amesema Rais Barack Obama hakuwepo White House na alipewa taarifa ya hali hiyo kwamba itatokea.
