
Mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu, pia utatumika katika kuitangaza promosheni ya Bahati Nasibu ya Jishindie Nyumba ambayo inaendeshwa na gazeti hili sambamba na magazeti mengine ya Global Publishers.
Nahodha wa Global FC, Philipo Nkini, ameliambia Championi Ijumaa kuwa licha ya mchezo huo kuwa wa kirafiki, lakini wao wanauchukulia kwa uzito.
“Huu ni mwanzo wa michezo yetu ya kirafiki ambayo kwa kipindi hiki itakuwa kila mara ambapo tumejiandaa vziuri kukabiliana na wapinzani wetu ambapo pia mchezo huu tutakuwa na kitengo chetu cha usambazaji ambacho kitadili na kuitangaza bahati ya Shinda Nyumba,” alisema Nkini.
