» »Unlabelled » Tanzania yatajwa kuathiriwa na sera za Trump

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zinaweza kuathirika kutokana na kuchaguliwa kwa Donald Trump kuwa Rais wa Marekani.

Hayo yalisemwa juzi Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Wahasibu katika nchi za Uingereza na Wales (ICEAW) Kanda ya Kati, Afrika na Asia ya Kusini, Michael Armstrong, wakati akizindua ripoti ya utafiti mpya uliofanyika ili kuangalia sera za kiongozi huyo zinavyoweza kuzisaidia ama kuziathiri nchi za Afrika.

Akizindua ripoti hiyo iliyopewa jina la Economic Insight: Africa Q4 2016, alisema dalili zinaonyesha kuwa hali hiyo itatokana na sera ya upanuaji wa matumizi ya fedha chini ya utawala wa Trump, pamoja na kupunguzwa kwa matumizi ili kukidhi ongezeko la miundombinu nchini Marekani.

“Misaada ni mojawapo ya vitu ambavyo vinaweza kuiathiri Afrika, kutokana na mabadiliko katika sera za Marekani chini ya uongozi wa rais mpya.

“Watunga sera na wafanyabiashara wana hamu kuona mipango ya sera za maendeleo za Rais mteule Trump atakapoingia ofisini,”  alisema.

Alisema utafiti huo ulifanywa na ICAEW wakishirikiana na taasisi ya uchumi ya Oxford (Oxford Economics) ili kutoa maelezo ya utendaji wa uchumi wa kanda, hasa nchi za Afrika.

Alizitaja nchi nyingine ambazo zinaweza kukumbana na janga hilo kuwa ni Kenya, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Ivory Coast, Afrika Kusini na Angola.

 Kwa mujibu wa Shirika la Kiuchumi, Ushirikiano na Maendeleo (OECD), Marekani ndiyo mfadhili mkuu wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Imekuwa ikitoa Dola bilioni tisa kila mwaka kwa kila kanda.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post