» »Unlabelled » Ratiba ya CAF imetoka Azam FC na Yanga SC kukutana na hizi timu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetoa ratiba ya mechi za awali za michuano ya klabu Afrika mwakani, Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Ngaya de Mbe ya Comoro.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam FC wao wataanzia Raundi ya kwanza ambako watamenyana na mshindi kati ya Mbabane Swallows ya Swaziland na Opara United ya Botswana.

Yanga wataanzia ugenini wikiendi ya Februari 10 hadi 12 kabla ya marudiano wikendi ya Februari 17 hadi 19, mwaka huu.

Azam wao wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 na marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.

Yanga wakivuka hatua hiyo watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia na APR ya Rwanda katika Raundi ya kwanza. Na Yanga wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 kabla ya marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.

Source: Binzubeiry

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post