Ukaguzi huo umefanyika hii leo alfajiri katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani ya Uganda kilichopo Nyegezi jijini Mwanza, ambapo Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa Mrakibu Mwandamizi wa polisi Robert Hussein aliongoza zoezi hilo la kupima kilevi kwa madereva wa mabasi,ukaguzi wa mabasi ya abiria na kutoa elimu kwa abiria kuhusu wajibu na haki zao wanapokuwa safarini.
Peter Rusibamayila ni balozi wa usalama barabarani mkoani Mwanza anasema kazi kubwa waliyonayo ni kuwaelimisha abiria ili waweze kupaza sauti, kutambua haki na wajibu wao ikiwemo kufunga mkanda kwa lengo la kupunguza ajali zinazoweza kuepukika,huku baadhi ya abiria na madereva wakishauri kuwa zoezi hilo linapaswa kuwa endelevu.