![](http://2.bp.blogspot.com/-IQBLrAI5ZR8/V2G0HuVs_SI/AAAAAAAAAx0/TigTDQ7X9Uk-pc008w18b4uyPcdys4W_QCK4B/s1600/SAX.gif)
Monday, December 26, 2016
Singida. Rais John Magufuli amesema sababu ya kuamua kusherehekea Krismasi kwenye Kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu mjini Singida imetokana na rozari aliyopewa na sista wa kanisa hilo ili imsaidie kushinda urais.
Alisema wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita, aliwahi kusali kwenye kanisa hilo na alipokuwa akitoka alikutana na sista mmoja ambaye hamkumbuki jina ambaye alimzawadia rozari na kumuahidi kuwa itamsadia kushinda urais.
Rais Magufuli akiwa na mkewe Janeth, alifichua siri hiyo alipozungumza kwenye ibada ya sherehe hiyo iliyofanyika jana asubuhi kanisani hapo.

![](https://4.bp.blogspot.com/--TVzeBRazc0/V2kJYL2MQ8I/AAAAAAAAD6w/vG9qlLA8mGUTbcEsL_RKLfKUg-1XBndjQCLcB/s1600/YOU.png)