» »Unlabelled » Chanzo, Athari, Kinga na Tiba ya Ugonjwa wa Manjano

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Monday, December 26, 2016

Ugonjwa    wa  Manjano    ambao  hufahamika  kitaalamu  kama  HEPATITIS  B  ni  hatari  sana  na umesababisha  vifo  vya  mamilioni  ya  watu  duniani  kote. 

Kwa  mujibu  wa  ripoti  ya  Shirika  la  Afya  Duniani  ( W.H.O )  kuna  zaidi  ya  wau  Milioni  350 duniani  ambao  wameathiriwa  na  ugonjwa  huu  hatari   kabisa  na  zaidi  ya  watu  620,000  hufa kila  mwaka  kwa  ugonjwa  wa  Manjano.

CHANZO   CHA  UGONJWA  WA  MANJANO
Ugonjwa  wa  Manjano  husababishwa  na  virusi  viitwavyo  “ Hepatitis  B “ (  HBV )  ambavyo  hushambulia    zaidi ini  la  mwanadamu.   Virusi  hivi  visipo  tibiwa  mapema  hutengeneza  uvimbe  katika  ini  na  kusababisha  asratani  ya  ini  ambayo  hupelekea  kifo.

MAMBO  YASABABISHAYO  MAAMBUKIZI  YA  UGONJWA  WA  MANJANO.
Ugonjwa  wa  Manjano  huambukizwa  kwa  njia  zifuatazo  :

  1. Kujamiiana  bila  kutumia  kinga.
  2. Kunyonyana  ndimi
  3. Kuchangia  damu  isiyo  salama
  4. Mama  mjamzito mwenye  ugonjwa  huu  anaweza  kumuambukiza  mtoto  wake  wakati  wa  kujifungua.
  5. Kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  vile  wembe  na  sindano.


DALILI  ZA  UGONJWA  WA  MANJANO
Dalili  za  ugonjwa wa  manjano  huchukua  muda  mrefu  kuonekana  tangu  maambukizi  yatokee, na  zinapo  anza  kuonekana  wazi  wazi, mgonjwa  anakuwa  amesha  athirika  kwa  kiwango kikubwa  sana.  Dalili  za  ugonjwa   huu  ni  kama  ifuatavyo :

  1. Uchovu  wa  mwili
  2. Kichefuchefu
  3. Mwili  kuwa  dhaifu
  4. Homa  kali
  5. Kupoteza  hamu  ya  kula
  6. Kupungua  uzito
  7. Kupatwa  na  maumivu  makali  ya  tumbo upande  wa  ini.
  8. Kukojoa  mkojo  wa  rangi  nyeusi
  9. Macho  na  ngozi  kuwa  vya  njano.

KINGA  YA  UGONJWA WA  MANJANO
  1. Kupatiwa  chanjo  ya  kujikinga  na  maambukizi  ya  ugonjwa  huu.
  2. Kutumia  kinga  wakati  wa  kujamiiana
  3. Kuacha   kuchangia  vitu  vyenye  ncha  kali  kama  sindano, wembe  n.k
  4. Kutochangia  mswaki
  5. Kuwa  na  mpenzi  mmoja  mwaminifu
  6. Kuto ongezewa damu  ambayo  haijapimwa  na  kuthibitika  kuwa  salama.


TIBA  YA UGONJWA WA MANJANO
Ugonjwa  wa  manjano  hauna  tiba  isipokuwa  mgonjwa   akiwahi  hospitali  atapatiwa  dawa za kupambana  na  virusi  kuvipunguza  nguvu  za  kupambana  na  ini., kupandikizwa  ini  ambapo ini lililoathirika  huondolewa  na  kuwekwa  jingine  japo  ni  vigumu  kupata  ini  salama.

Ukisha  gundua  kuwa  umeambukizwa  ugonjwa  huu  unashauriwa   kuacha  kutumia  pombe, dawa za kulevya  na  vitu  vingine  vinavyo  athiri  utendaji  kazi wa  ini.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post