» »Unlabelled » Ziara ya Shaka yazua jambo kwenye jimbo la CHADEMA

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamidu Shaka akiwa ananyesha baadhi ya kadi za chadema ambazo zilirudishwa

Ziara ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, wilayani Simanjiro, imezua jambo baada ya Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, James Ole Millya (Chadema), kuchachamaa akidai amekwenda kinyume na agizo la Rais la kuzuia mikutano ya hadhara ya siasa

Inadaiwa kuwa Shaka alifanya mikutano ya hadhara ya siasa katika Kijiji cha Loiborsoit A, kilichopo Kata ya Emboret hivi karibuni.

Katika madai yake jana, Ole Millya amesema anashangazwa na Shaka kufanya siasa kwenye kijiji hicho ili hali siyo diwani wa kata hiyo au Mbunge wa Jimbo hilo wakati Rais Magufuli alipiga marufuku.

Amesema baadhi ya wananchi na viongozi wa kijiji na kata hiyo walimpigia simu na kumweleza juu ya kiongozi huyo wa UVCCM, kuvamia eneo lao na kufanya mkutano wa hadhara ili hali Rais anayetokana na CCM alipiga marufuku suala hilo.

 Amesema baada ya kupata taarifa hizo atazungumza na viongozi wa chama chake ili watoe tamko kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, Katibu wa UVCCM Wilayani Simanjiro, Bakari Mwacha, amesema Shaka alizungumza katika Kijiji cha Loiborsoit A kwa kuwa mkutano huo ulikuwa ni wa diwani wa Kata ya Emboreet, Christopher Kuya, akiutumia kusoma taarifa ya maendeleo.


Amesema Shaka alikuwa na ziara ya siku mbili wilayani humo ikiwemo kuzindua jengo la ofisi ya UVCCM wilaya ya Simanjiro, kupokea wanachama wapya wa jumuiya za UVCCM, UWT, wazazi na wa CCM.

Kamanda wa UVCCM wilayani Simanjiro, Daniel Ole Materi, amesema ziara ya Shaka kwa namna moja au nyingine imefanikisha kurejesha uhai wa jumuiya hiyo, kwani vijana wametiwa hamasa na ushauri mzuri wa maendeleo yao. 


ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post