HIRIKA la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), limesema kuwa kuwawezesha wanawake kunahitaji juhudi mpya na za ziada katika kumaliza vitendo vya ukatilli na unyanyasaji.
Mkurungezi wa UNFPA, Dk. Babatunde Osotimehin, alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati wa maandamano yatakayoanza leo ya siku 16 ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake.
Alisema kwa mwaka huu kila mwanamke mmoja kati ya watatu wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kimwili au wa kingono na mtu anayemjua.
“Mamilioni ya wanawake na wasichana wamekutana na aina nyingi za unyanyasaji na ukatili kama ukeketwaji ambao umeathiri zaidi ya wanawake na wasichana milioni 200 duniani. Pia suala la ndoa za utotoni limewaathiri kwa sababu msichana mmoja kati ya watatu huolewa chini ya miaka 18 katika nchi zinaoendelea,” alisema.
Aliongezea kuwa unyanyaji pia umechangia matatizo ya kiafya ya kudumu ikiwamo ulemavu, mimba zisizotarajiwa, matatizo ya akili na utoaji mimba usio salama.
“Kulinda wanawake na wasichana dhidi ya ukatili na unyanyasaji, si tu kwamba ni suala la haki za binadamu, bali pia ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya mataifa,” alisema Osotimehin.
Osotimehin alielezea pia kuwa kila siku, mamilioni ya wanawake na wasichana wanarudishwa nyuma kimaendeleo kutokana na unyanyasaji ambao huwazuia kuwa na uwezo bora wa kufikiri katika maisha.
Shirika la UNFPA jukumu lake ni kuondoa ukatili wa kijinsia duniani kote, hasa katika nchi zilizoathirika na vita au majanga na zile zenye hatari ya ukatili dhidi ya wasichana na wanawake.
Mwaka jana pekee mfuko wa UNFPA uliwekeza zaidi ya Dola za Marekani milioni 93 za kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vya kikatili katika nchi zinazoendelea na migogoro ya kibinadamu.
Maadhimisho ya siku ya kuondoa unyanyasaji dhidi ya wanawake hufanyika Novemba 25 kila mwaka.