» »Unlabelled » Mapigano ya kikabila yasababisha vifo Jamhuri ya Afrika ya Kati

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Watu 4 wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia mapigano ya kikabila yaliyozuka miongoni mwa wanachama wa zamani wa kundi la silaha la Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Afisa mkuu wa vikosi vya usalama Inus Ngabdjia aliarifu kuzuka kwa mapigano hayo kati ya wafuasi wa Nureddine Adam wa upande wa FPRC na wafuasi wa Ali Ndarass wa upande wa UPC.

Mashuhuda wa tukio hilo wamearifu kuuawa kwa watu 4 kwenye mapigano hayo, na kujeruhiwa kwa wengine 14.

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kusitisha mapigano hayo kupitia vikosi vya MINUSCA, huku wakilaani mashambulizi yaliyotekelezwa dhidi ya kambi zao nchini humo.

Tangu Desemba mwaka 2012, nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na mizozo kati ya kundi la Seleka la wafuasi wa Kiislamu na anti-Balaka lenye wafuasi wa Kikristu.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post