» »Unlabelled » Anayetuhumiwa kuchinja kizimbani

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Sadick Andrea amepanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Muheza, akikabiliwa na shtaka la kumuua ya mke wake, Tabu Meyson kwa kumchinja shingoni na kisu.

Mshitakiwa huyo alisomewa shitaka lake juzi mbele ya Hakimu wa Wilaya, Enediana Makabwa katika mahakama ambayo ilijaa umati wa watu kutoka ndani na nje ya Muheza, wakiwamo ndugu wa marehemu huyo, pamoja na kuwapo kwa ulinzi mkali wa polisi.

Ilidaiwa mahakamani hapo kwamba mtuhumiwa alimchinja mke wake shingoni katika kijiji cha Ngarani B, katika kata ya Kwakifua wilayani Muheza mkoani Tanga na kumuua.

Hata hivyo, kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji, Andrea hakutakiwa kujibu lolote. Kesi yake itahamia Mahakama Kuu upelelezi utakapokamilika.

Mshitakiwa alirudishwa rumande mpaka Desemba 6 kesi hiyo itakapotanjwa tena.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post