Wananchi wa Ivory Coast wameanza mchakato wa kupiga kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya iliyowasilishwa na rais Alassane Ouattara.
Rasimu hiyo ilipitishwa bungeni na mapema wiki jana ambapo inapendekeza kuwepo kwa nafasi mpya ya naibu wa rais atakayeteuliwa na rais pamoja na baraza seneti.
Viongozi wengi wa upinzani wamekuwa wakipinga mabadiliko hayo ya katiba kwa kudai kuwa rais Ouattara analenga kumteua mrithi wake atakayechukuwa uongozi baada ya kukamilisha muhula wake mwaka 2022.
Takriban watu milioni 6.3 wamepewa haki ya kupigia kura ya maoni rasimu ya katiba hiyo.
Jumla ya vituo 20,000 vya kupiga kura vitafunguliwa kote nchini kuanzia saa 8.00 asubuhi hadi saa 18.00 jioni.
Matokeo ya kura ya maoni yanatarajiwa kutangazwa rasmi siku ya Jumatatu au Jumanne.