Jumla ya watahiniwa 408,442 wa kidato cha nne wanatarajia kuanza mitihani ya kidato cha nne itakayoanza kesho, ikiwa ni idadi pungufu ya waliofanya mtihani huo mwaka jana.
Akizungumza na wanahabari leo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dk Charles Msonde amesema mwaka jana kulikuwa na watahiniwa 448,382 waliofanya mitihani huo.
Dk Msonde amesema maandalizi yote ya mitihani hiyo itakayomalizika Novemba 18, mwaka huu yameshakamilika.
Amewataka wanafunzi, walimu na wasimamizi kujiepusha na udanganyifu wa mitihani kwani baraza hilo halitasita kuchukua hatua za kisheria, ikiwamo kuwafutia matokeo.