» »Unlabelled » Lord Eyes: Ni muda mrefu sijaonana na Ray C wala hatuongei ila namuombea

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Msanii wa kundi la Weusi, Lord Eyes ambaye pia zamani alikuwa mpenzi wa Ray C amesema ana muda mrefu hajaonana na Ray C ambaye kwa sasa anapambana kuachana na matumizi wa Madawa ya kulevya.

Rapa huyo mwenye makazi yake mkoani Arusha, amesema anamuombea mwanadada huyo kwani kwa matatizo aliyonayo ni kama maradhi hivyo hayaponi kwa siku moja.

“Sijakutana naye wala hatuongei ila namuombea Mungu kwani tatizo lile ni kama maradhi mengine hivyo haliwezi kuisha kwa mara moja linachukua muda, anahitaji maombezi na mimi namuombea kama navyojiombea mimi nifanye kazi zikamilike tukutane kwenye show huko” Lord Eyez alikiambia kipindi cha Enewz cha Eatv.

Pia Lord Eyez amesema bado anaona Ray C ana nafasi ya kufanya vizuri kwenye muziki kwa kuwa hakuna msanii kwenye muziki anayefanya muziki wa aina yake.

“Leo hii kwenye muziki hatumuoni mtu kama Ray C, mpaka sasa hakuna mtu kama Ray C hivyo chumba chake kwenye muziki bado kipo kinamsubiri arudi tu,” alisema Lord Eyez.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post